Michezo ya marudiano ya robo fainali ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018 imeendelea tena usiku wa April 10 kwa michezo miwili kuchezwa, Man City ambao walifungwa mchezo wa kwanza 3-0 waliwakaribisha Liverpool wakati AS Roma walikuwa wenyeji wa FC Barcelona ya Hispania.
AS Roma leo wakiwa nyumbani wameushangaza ulimwengu baada ya kupindua matokeo na kuitoa FC Barcelona katika hatua ya robo fainali ya UEFA Champions League, mchezo wa kwanza wa Roma dhidi ya Barcelona uliyochezwa Nou Camp ulimalizika kwa Barcelona kupata ushindi magoli 4-1, hivyo Roma kupata ushindi wa magoli 3-0 leo kumewafanya wafuzu hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya magoli 4-4 ila goli la ugenini ndio linawabeba.
Magoli ya leo ya AS Roma katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Barcelona yalifungwa na Eden Dzeko dakikaya 6, Daniele De Rossialiyefunga goli dakika ya 58 kwa mkwaju wa penati na goli la mwisho likafungwa na Kostantinos Manolas dakika ya 82, AS Roma wanafanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza toka msimu wa 1983/1984 waliposhiriki kwa mara ya mwisho.