Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya mechi Simba vs Mbao, ‘mnyama’ anaingia uwanjani kuikabili mbao akiwa na rekodi ya kutopoteza mchezo tangu kuanza kwa msimu huu, Simba imecheza mechi 18 hadi sasa na kushind michezo 12, na kutoka sare katika michezo sita.
Mwenyekiti wa klabu ya Mbao Solly Njashi amesema, rekodi ni kitu ambacho kinaweza kikavunjwa dakika yoyote, timu yake imejiandaa kwa ajili ya kushinda mechi yao dhidi ya Simba.
“Rekodi ni kitu ambacho kinaweza kikavunjwa dakika yoyote, inaweza ikaendelea au ikavunjwa hilo ni suala la kawaida katika mpira. Kila kitu kipo tayari, sisi tumejiandaa kushinda mechi”-Solly Njashi, mwenyekiti Mbao FC.
Mbao FC imecheza mechi 18, imeshinda michezo minne, imetoka imepoteza michezo saba, na kutoka sare kwenye michezo saba. Imefanikiwa kupata pointi 19 katika mechi zake 18 ilizocheza hadi sasa.