Video iliyowanasa Dogo Janja na Irene Uwoya wakipelekana saloon


Kati ya vitu ambavyo havijashuhudiwa na watanzania wengi hususani wale wapenda burudani ni pamoja na picha au video za pamoja za staa kutokea kwenye bongofleva Dogo Janja na mke wake ambaye ni muigizaji Irene Uwoya baada ya kuowana.

Dogo Janja alishawahi kuzungumza kupitia millardayo.com na kusema kuwa mapenzi yake na mkewe Irene Uwoya ni private sana japo wanaweza kuongozana kwenda mahali popote na mkewe, kama Dukani na sehemu nyinginezo.

January 6, 2018 imesambaa video ikiwaonesha Dogo Janja na mkewe Irene Uwoya wakisindikizana saloon,Irene Uwoya na Dogo Janja wameoneka kwenye video wakiwa pamoja saloon ya kike ambapo inaaminika kuwa Dogo Janja alimsindikiza Irene Uwoya  kutengeneza nywele na inawezekana hii ndio ikawa video ya kwanza kuwaonesha wawili hawa wakiwa pamoja baada ya kuoana.
Unaweza kutazama video yenyewe hapa chini kwa kubonyeza PLAY

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post