Mti wa kale ambao umekuwepo Ikulu ya Marekani kwa karibu miaka 200 utakatwa.
Mti huo unaofahamika kama "Jackson" magnolia ulipandwa na rais Andrew Jackson kama kumbukumbu kwa mke wake.Umekuwa ukionekana kwa picha wakati wa sherehe nyingi huko White House na hata picha zake ziliwekwa kwenye noti za dola 20 kati ya mwaka 1928 na 1988.
Lakini wataalamu wanasema kuwa mti huo umeharibiwa na kuwa hatari kwa usalama. Mke wa Trump Melania Trump ametaka sehemu kubwa ya mti huo kukatwa.
Msemaji wa White House Stephanie Grisham anasema Bi Trump alichukua hataua hiyo kwa sababu mti huo ulikuwa ni tisho kwa usalama wa wageni na waandishi wa habari ambao mara nyingi husimama mbele yake wakati helikopta ya rais inapaa.
Mtu wa Magnolia ulipandwa kutoka ya mti wa magnoalia uliokuwa ukipendwa na Rachel Jackson katika shamba lao huko Tennessee.
Marais 39 wamehudumu mti huo ukiwa White House na pia ulikuwepo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani na vita vya kwanza na vya pili vya dunia.
Tags
Kimataifa