HIZI HAPA TIMU ZINAZOIKOSESHA USINGIZI YANGA TPL



MWINYI Zahera Kocha Mkuu wa Yanga amebakiwa na mechi sita mkononi kwa sasa ili kukamilisha Ligi Kuu msimu huu kabla ya kuanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.

Zahera kesho atamenyana na Azam FC uwanja wa Uhuru ikiwa ni mchezo wake wa kwanza msimu huu kutumia uwanja huo amesema kuwa hana hofu ya kupambana na timu iliyo ndani ya 10 bora badala yake anahofia kupambana na timu zilizo chini.

Zahera amesema kuwa amekuwa akiwaambia wachezaji wake kwamba kuna ugumu wa kupambana na timu zilizo chini ya msimamo kutokana na kupania ili zijinusuru na hali ya kushuka daraja.

"Ligi inakamalika ila huwa nakuwa sina hofu na timu ambazo zinafanya vizuri hizo napenda kucheza nazo kwa kuwa mbinu huwa zinafanana ila shida ipo kwenye timu ambazo zipo nafasi ya chini.

"Kupambana na timu ambayo ipo nafasi ya chini kunahitaji umakini mkubwa kwani wao hesabu zao ni kupata matokeo na wanatumia nguvu nyingi na kasi hali ambayo inafanya ushindani kuwa mkubwa, hivyo nami huwa nabadili mbinu kukabiliana nao," amesema Zahera.

Timu ambazo zitacheza na Yanga na zipo nje ya kumi bora ni pamoja na Biashara United ipo nafasi ya 19 na Ruvu Shooting ambayo ipo nafasi ya 18 huku zile ambazo zipo ndani ya 10 bora ni pamoja na Azam FC nafasi ya 3 Tanzania Prison iliyo nafasi ya 8  na Mbeya City ipo nafasi ya 10.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post