SHOMARI KAPOMBE AANZA MAZOEZI RASMI SIMBA



Beki wa klabu ya Simba SC, Shomary Kapombe aameanza mazoezi mepesi baada ya kukaa nje ya dimba kwa muda kutokana na kupata majeraha mguuni.

Kapombe ameanza mazoezi hayo ikiwa ni baada ya kupona majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania huko Afrika Kusini.

Beki huyo wa kupanda na kushuka alipa majeraha hayo wakati Taifa Stars ikijiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho.

Kapombe kwa sasa anafanya mazoezi ya GYM kurudisha mwili katika hali yake ya kawaida.

    

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post