#Ruge_Mutahaba anaandika;
"Nimefikiria sana. Nahisi ni wajibu wangu kuandika kwenu wasanii maana Jana tulikuwa na kikao kirefu cha kupanga mikakati ya show, na Leo minong'ono iko kila mahali kutokana na alichosema RC asubuhi. Ukiniuliza tunafanya nn?? Nitasema sina jibu.
Ukiniuliza najisikiaje nitakwambia roho inauma sana....sio kwa hiyo kauli ila nikiwaza hii chuki dhidi yangu kwann inaumiza wengine. Namuwaza mtoto wa Roma, Ivan, mtoto wa barnaba, mamaake na Darasa, ndugu, jamaa na wazazi wanaofaidika na kipato cha kazi yenu ya Sanaa.
Tutapunguza nusu ya wasanii kwenye ratiba, najiuliza wanadhani wanamkomoa Ruge kweli?????? Kwann wasinichukue wakaniweka ndani siku 2 au 3 wasuuze mioyo yao kuliko kugusa maisha ya watu wadogo wanaotafuta.
Miaka 17 ya kuhangaika Muziki wa Tanzania usimame wenyewe na upate heshima wenyewe ndo mwaka huo huo sanaa inavuliwa nguo. Kwa hiyo kwa miaka 16 ya wasanii wa nje tulipiga mpaka asubuhi Leo tumebaki wa Tanzania wenyewe, tunaambiwa hatustahili hii heshima.
Mi nawaomba wote hata kama tutapewa one hour, we will perform hata kwa dakika 5 each and Historia itaandikwa.
Kizingiti kisichokuua kinakufanya uwe imara zaidi. Mi nitaendelea kupigania sanaa ya Bongo....hata matamasha yakifungiwa tutarekodi na kuuza muziki.