Breaking News: Lulu Michael Kwisha Habari yake...Apigwa Mvua Miaka Miwili Jela



 
HUKUMU: Mahakama Kuu imemhukumu Mwigizaji wa Filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu kwenda jela miaka 2 kwa hatia ya kuua bila ya kukusudia.
.
Lulu alikuwa akikabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba mwaka 2012.
.
Elizabeth Michael kwa Mara kwanza alipelekwa Mahakama ya kisutu iliyopo Dar es salaam, akishtakiwa kuua bila kukusudia tarehe 7 mwaka 2012" "Ushahidi wa mazingira ni ushahidi ambao mstakiwa alikubali kwamba yeye ni MTU wa mwisho kuwa na marehemu ambapo mshtakiwa alikuwa na mahusiano na marehem kwa miezi 4"
.
Ushahidi wa mazingira unaweza kutumika kama msingi pekee wa kumtia hatiani mshtakiwa tena mshtakiwa pekee, Sasa ninapokwenda kuangalia maelezo ya mshtakiwa kama yanakidhi vigezo nilivyosema awali" "Kwa mujibu wa mshtakiwa alisema alianza kupigwa na marehem, Mshtakiwa alisema kuwa marehemu alilewa lakini kuhusu mshtakiwa anatakiwa kutoa Maelezo yanayo jitosheleza kwa hili mshtakiwa alijikanganya"
.
Mshtakiwa katika maelezo yake hakueleza kuwa marehemu alianguka au laah!! wakati anamkimbiza, Maelezo ya Dkt. Josephine siyo maelezo ya cheti cha hospitali hayakuwa na hadhi ya hospitali" "Inakinzana na hekima ya kawaida kwamba hata pale marehemu alipoendelea kumpiga na kumshambulia na akaenda kiwango cha kumtishia kumuua, mstakiwa hakuthubutu hata kumpiga..." Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia na hukumu itatolewa baada ya mawakili wake kujitetea.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post