Mwigizaji Elizabeth Michael “Lulu” leo amehukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia na kusababisha kifo cha Mwigizaji Steven Kanumba.
Baada ya Hukumu hiyo kutolewa Mama Mzazi wa Marehemu Kanumba aliangua kilio na kuongea yafuatayo >>> “Namshukuru Mwenyenzi Mungu, naishukuru Mahakama imetenda haki, naishukuru Serikali yangu awamu ya tano“
“Kalale salama mwanangu Steven Kanumba na nikitoka hapa nakwenda makaburini naamini nakwenda kumzika akapumzike kwa amani” – Mama Kanumba
Tags
Urembo