Faida za Kuwajali na kuwaheshimu Wazazi wetu

EWE MOLA WAREHEMU (WAZAZI WANGU) KAMA WALIVYONILEA NIKIWA MTOTO MCHANGA.

Ameamrisha Allah mtukufu juu ya kuwajali, kuwaheshimu, kuwatunza na kuwatii wazazi wawili.

وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئاً وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانا.

Muabuduni Mwenyezi Mungu wala musimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili (Annisaai 36).

وَقَضَى رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانا.

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa musimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema.(Al-lsraai 26).

وَوَصَّيْنَا الْأِنْسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَاناً حَمَلَتْهُ أُمُّهُ كُرْهاً وَوَضَعَتْهُ كُرْها.

Na tumemuusia Mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu (Al ahqaaf 15).

إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِنْدَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُلْ لَهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُلْ لَهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا

Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshima (Al - lsraai 23).

Maneno ya Mtume swalla llaahu alayhi wasallama juu ya wazazi.

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ،إثنان يعجّل هما الله في الدّنيا: البغي وعقوق. الوالدين( رواه الطبرني).

Amesema Mjumbe wa Allah swalla llaahu alayhi wasallama, Watu namna mbili huwafanyia haraka Allah (kuwaadhibu) duniani, Umalaya na kuto watendea haki wazazi wawili (Ameipokea Twabraaniy).

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم، كلّ الذّنوب يؤخّر الله منها ما شاء إلى يوم القيامة، إلا عقوق الوالدين فإنّ الله يعجّله لصاحبه في الحياة قبل الممات ( رواه الحاكم).

Amesema Mjumbe wa Allah swalla llaahu alayhi wasallama,, Kila madhambi huyachelewesha Allah namna atakavyo mpaka siku ya Kiama, ila kutowatendea haki wazazi wawili, hakika Allah humuadhibu haraka mfanyaji wake katika uhai kabla ya kufa ( Ameipokea Alhaakim).

عن أبي هريرة : أنّ رجلاً جاء إلى النّبي - صلّى الله عليه وسلّم - فقال ، يا رسول الله، من أحقّ النّاس بحسن صحابتي؟ قال: أمّك، قال: ثمّ من؟ قال: أمّك، قال:ثمّ من؟ قال: أمّك، قال: ثمّ من ؟ قال: أبوك (رواه البخاري)

Amesimulia Abuu Hurairah, Hakika mtu alikuja kwa Mtume swalla llaahu alayhi wasallama akauliza, Ni nani mweye haki katika watu nishikamana nae vizuri? Akasema mama yako, akauliza kisha nani? Akasema mama yako,,akauliza kisha nani? Akasema mama yako, akauliza kisha nani? Akasema baba yako ( Ameipokea Bukhari).

أنّ النّبي - صلّى الله عليه وسلّم - قال:ألا أنبّئكم بأكبر الكبائر؟ ثلاثاً، قالوا: بلى يا رسول الله، قال: الإشراك بالله، وعقوق الوالدين،(رواه البخاري)

Hakika Mtume swalla llaahu alayhi wasallama amesema, Hivi nikuambieni dhambi kubwa katika madhambi makubwa yenye kuangamiza? Wakasema ndiyo tuambie ewe Mjumbe wa Allah, Akasema ni kumshirikisha Allah na kutowatendendea haki wazazi wawili. (Ameipokea Bukhari).

Mambo yanayo dhihirisha, kuwadharau, kutowajali, kuwapuuza na kutowathamini wazazi wawili.

(a) Kufanya kwa makusudi yale yenye kuwahuzunisha nafsi zao na kuwaliza iwe kwa maneno au vitendo.

(b) Kuinua sauti juu yao na kuwapuuza kwa vitendo au kauli kama kuwakaripia n.k.

(c) Kutowasaidia kazi za nyumbani kama usafi, kuteka maji, kupika, kufuga, kulima n.k.

(d) Kuwakunjia uso au kuwakebehi wakati wa kuzungumza nao.

(e) Kutozungumza nao au kuwaongopea, au kubishana nao na kutojifanya mdogo mbele yao.

(f) Kuwatenga kwa kuwadharau na kuwashusha hadhi kutokana na umaskini wao au maumbile yao duni kama ulemavu n.k.

(g) Kutokubali ushauri wao au kuomba ushauri kwao katika mambo kama kuoa au kuolewa, Talaka, au kuhama nyumbani kwa wazazi wako bila ruhusa yao na kuhamia sehemu nyingine.

(h)Kufanya mambo mabaya yenye kuchukiza mbele yao, iwe kwa mkeo au mumeo au nduguyo au mtu yeyote yule.

(i) Kuwapinga wazazi mbele za watu, au kuwakejeli, au kutaja aibu zao, au sifa zao mbaya kama kusema, Baba yangu ni mchawi au mzinifu n.k, au hakunilea vizuri utotoni, yeye ni sababu ya mimi kuwa hivi nilivyo.

(j) Kuwatukana na kuwalaani pamoja na kuwashutumu kama anavyo tukana mtu kumtukana mzazi wa mwenziye basi ajue amejitukania mzazi wake maana na yeye hatonyamaza atamrudishia.

عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما، أنّ رسول الله - صلّى الله عليه وسلّم - قال:من الكبائر شتم الرّجل والديه. قيل: وهل يشتم الرّجل والديه؟ ! قال: نعم! يسبّ أبا الرّجل فيسبّ أباه، ويسبّ أمّه فيسب أمّه(رواه البخاري.)

Amesimulia bnu Umar Allah awaridhie, Hakika Mjumbe wa Allah swalla llaahu alayhi wasallama amesema, Katika madhambi makubwa ni mtu kumtukana mzazi wake, Pakaulizwa, hivi mtu atamtukanaje mzazi wake?. Akasema ndiyo (yawezekana) Anamtukana baba wa mtu na yeye anamtukania baba yake, anamtukania mama yake na yeye anamtukana mama yake ( Bukhari).

(k) Kuingiza vitu vyenye kuwakera ndani ya nyumba kama mahawara, ala za muziki, picha za ngono au kuwafundisha tabia mbaya nduguzo kama wizi au uzinifu n.k.

(l) Kujionesha mbele ya wazazi wako ukiwa amelewa pombe, au kulala muda wa Swala, au kuingiza marafiki waovu nyumbani mwao, na haya yanadhihirisha kuto kuwa na adabu na ukosefu wa haya kwa wazazi wako.

(m) Kutowasikiliza kwa kujihusisha na kazi mbaya kama Umalaya, Ujambazi, Kuuza madawa ya kulevya, kuuza pombe, Ushoga n.k, yote haya huwakoseha raha wazazi.

(n)Kujiweka mbali na wazazi bila ya kuwatembelea au kuwajulia hali zao ikawa ni sababu ya kuingiwa khofu juu ya mtoto wao kwa kutojua huko aliko ni hai au amekufa!!!??

(p)Mke wako kutowajali wazazi wako ikawa ni sababu ya kukosa haki zao kwako kwa ajili yake, na wewe ukajifanya kama huyaoni kwa kutawaliwa na huyo mkeo.

(q) Kujitia mishughuliko sana ikawa huendi kuwaona wazazi wako nao ni vikongwe, hata kama unawapa huduma, tabia hiyo haliwaridhishi kwani nao wanahitaji kumuona mtoto wao.

(r)Kutopenda watu wajue kwamba hao ni wazazi wako ikawa unaficha huku ukijipa nasaba nyingine kutokana na unyonge wao na wewe ukajiona ni mwenye hadhi nao hawapendezi kuwa ni wazazi wako.

Nasaha zangu juu ya kadhia hii.

Kama una watoto kumbuka jinsi unavyo hangaika na nafsi yako pindi mtoto wako anapo ugua, basi ni hivyo hivyo ilivyo kuwa kwa wazazi wako juu yako pindi ukiugua, ilikua hawalali kwa ajili yako, hawafurahi kwa ajili yako, leo unawapuuza, ama kweli mabalaa mengine ni kujitakia.

Kama mzazi wako yuko hai na kuna mambo umemkwaza, wahi mapema akiwa hai umtake radhi, Usisubiri kaburi, kwani kaburi haliombwi msamaha.wengi wameharibikiwa kwa kuwadharau wazazi wao.

Elimu ndio kazi yetu na Tawfiyk ni ya Allah hivyo penda kutembelea account na page yetu ya facebook ya Uislamu kitabu na sunnah na jiunge na group la facebook la Uislamu Sahihi ni Qur'an na Sunnah.

Ewe Mola, tujaalie tusiwakwaze wazazi wetu, na yale tuliyo wakwaza tunaomba utusamehe

2 Comments

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post