KISINDA NI MCHEZAJI HALALI WA YANGA, MKWANJA WATAGAWANA NA AS MANIEMA

 


 MENEJA wa mchezaji wa Yanga, Tuisila Kisinda anayeitwa Nestori Mutuale amesema Klabu ya RS Berkane ilituma ofa kwa Klabu ya Yanga ili kuipata saini ya Tuisila Kisinda .


Mutuale amesema Kisinda alisajiliwa na Yanga akitokea As Maniema ya Dr Congo ambayo itapata mgawo wa asilimia kadhaa katika fedha itakayopatikana kutokana na mauzo ya Kisinda.

Yanga wameeleza kuwa wamepokea ofa kutoka timu hiyo ya Morocco ambapo dau lililowekwa mezani ni nono na ofa ya kuelekea nchini humo kuweka kambi kwa ajili ya msimu wa 2021/22.

Ilikuwa ikielezwa kuwa Kisinda hakuwa mchezaji wa Yanga alikuwa hapo kwa mkopo jambo ambalo meneja huyo amelikana.

"Kisinda alisajiliwa na Yanga kwa kuwa waliingia makubaliano na AS Maniema ambapo alikuwa akicheza AS Vita kwa mkopo hivyo yeye ni mchezaji halali wa Yanga na hayupo hapo kwa mkopo.

"Kwa kuwa ni mali ya Yanga basi hata ofa ya mchezaji huyo imefika kwa Yanga ambao watapata mgawo na watawapa mgawo pia waajiri wake wa zamani," amesema.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post