KMC YASAINI DILI LA MIAKA MIWILI NA MASITA

 


 KLABU ya Manispaa ya Kinondoni,(KMC FC) leo Agosti 11 imesaini mkataba wa miaka miwili na kampuni ya kusambaza vifaa vya michezo duniani Masita Sports Wear ya nchini Uholanzi kwa ajili ya kusambaza vifaa vya timu.

Dili hilo ambalo limesainiwa leo mbele ya waandishi wa habari ni la muda wa miaka miwili.

Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dar Es Salaam chini ya Kampuni ya Level Up ambao ndio wawakilishi wenye hati miliki ya kusambaza vifaa vya Masita kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Level Up Mr Daud Aboud amesema ni nafasi kubwa kwao kuweza kufanya kazi na timu kubwa kama KMC FC na wana imani wataweza kushirikiana vizuri katika makubaliano hayo na kuweza kutimiza lengo la kuhakikisha wanaleta vifaa bora vinavyotengenezwa na kampuni ya MASITA.

Katibu Mkuu wa KMC FC, Walter Harson amesema MASITA ni kampuni bora na wanategemea ubora zaidi utaongezeka baada ya kufanya kazi kwa msimu uliopita kwa kiwango kikubwa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post