Nahodha wa klabu ya Simba SC, John Bocco amemuandikia ujumbe boss wao ambaye ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Mo Dewji na kumshukuru kwa zawadi ya Ubingwa waliyoupata.
Bocco ameandika ujumbe huo kwenye akaunti yake ya kijamii ya Instagram
”Ulistahili kupokea hii zawadi @moodewji ukiwa kama mwenyekiti wetu na muwakilishi wa wanasimba wote @simbasctanzania niwashukuru mashabiki wetu kwa umoja wenu na upendo kwa sisi wachezaji wenu🙏🏿🙏🏿 niwashukuru sana viongozi wetu kwa juhudi maarifa na mazingira mazuri wanayotuwekea sisi wachezaji ilikuifanya kazi yetu vizuri @bvrbvra 🙏🏿🙏🏿🙏🏿 @moodewji pokea asante yetu boss tunathami sana moyo wako na mazingira mazuri ya kazi unayotuwekea boss pamoja na bodi yako kwa ujumla🙏🏿🙏🏿🙏🏿 @simbasctanzania umoja wetu na upendo wetu ndio nguzo ya sisi kufanya vizuri zaidi kwa msimu unaokuja🦁 niwakati wakuzidisha imani,upendo na umoja kwa wachezaji,benchi la ufundi pamoja na viongozi wetu ili tuzidi kupata mafanikio makubwa zaidi kwa misimu ijayo💪🏿 @hajismanara nikushukuru kaka kwa kuitumikia club yetu nakutakia kheri kwa kila jambo kaka mkubwa🦁nguvumoja🦁”- Ujumbe wa John Bocco