Mshauri wa timu za vijana nchini, Kim Poulsen, ameamua kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kumlipa stahiki zake ikiwemo mshahara.
Taarifa zimeeleza Poulsen amekuwa akifanya kazi hiyo lakini amekosa mshahara kwa miezi kadhaa hivyo kupelekea kuamua kuandika barua kuomba kuachia ngazi ili kuwapa nafasi watu wengine.
Mbali na kutolipwa mshahara, imeelezwa pia Poulsen alipunguziwa mshahara katika utawala huu wa sasa tofauti na aliokuwa akipewa wakati wa Jamal Malinzi hivyo nayo inatajwa kama sababu mojawapo ya yeye kujizulu.
Kutokana na kujizulu kwa Poulsen, nafasi yake kwa sasa ipo wazi hivyo itabidi atafutwe mbadala mwingine ili kuziba pengo lake kwa ajili ya kuendeleza soka la vijana hapa nchini.
Tags
Michezo