Mapenzi Mazuri Ni Yale Yanayowakutanisha Wapendanao Wawili, Ambao Wanaelewana, Wanasikilizana Na Kufurahia Wakati Mzuri, Pia Kuhuzunika Pamoja Katika Wakati Wa Majonzi.
Kukutana Na Mtu Mnayeendana Ni Mtihani, Kidogo. Wapo Ambao Wanasukumwa Na Matamanio Ya Kimwili Na Matokeo Yake, Wanajikuta Kwenye Wakati Mgumu Penzini Kutokana Na Kuanzisha Uhusiano Na Mtu Ambaye Kwa Namna Moja Au Nyingine, Hawaendani.
Suala La Kujiuliza Hapa Utampataje Mwenza Sahihi? Nini Cha Kufanya Ili Uweze Kumpata Mtu Sahihi? Hapa Ndipo Wengi Wanapokosea Hususan Wanaume. Wanajikuta Wanalazimisha Mambo Ambayo Kimsingi Hayahitaji Kulazimishwa.
Wanaume Wana Kasumba Ya Kulazimisha Au Kujipa Jukumu La Mwisho La Uamuzi. Kwamba Anapojiridhisha Yeye Kwa Vigezo Na Sifa Yake Kwa Mwanamke Fulani, Basi Anaamua Kuwa Naye. Kwa Namna Yoyote, Atamtaka Huyo Mwanamke Awe Wake.
Yaani Hampi Nafasi Huyo Mwanamke Naye Afanye Tathimini Zake Kwake, Anamlazimisha Amkubali Na Ikiwezekana Amuoe. Mwanamke Awe Amejiandaa Kuolewa Au Hajajiandaa, Anamtaka Tu Akubaliane Na Maamuzi Yake.
Marafiki Zangu Hususan Wanaume, Katika Hili Tunakosea Sana. Wewe Kama Umefanya Tathimini Zako, Umemuona Mwanamke Fulani Anakufaa, Basi Huna Budi Naye Kumpa Nafasi Ya Kufanya Tathimini Zake Kabla Ya Kukubali.
Japo Kiasili Wanaume Ndiyo Mara Nyingi Wanaowaanza Wanawake, Lakini Isiwe Sababu Ya Kuwafanya Wanawake Na Wao Kutokuwa Na Uhuru Wa Kuwakubali Au Kuwakataa Wanaume. Wanaume Tuache Ubinafsi, Tutoe Nafasi Kwao.
Yawezekana Ukawa Unaamini Anafaa Kuwa Mke Wako Lakini Kwa Vigezo Anavyoviangalia, Yeye Akaona Wewe Haumfai Kuwa Mume Wake. Kumbe Anaweza Kukutathimini Na Kuona Wewe Hufai Kuwa Mume Wake, Hivyo Hata Ukilazimisha Vipi Haiwezi Kusaidia.
Wakati Mwingine Yawezekana Mwanamke Akawa Na Mtu Wake Mwingine Anayempenda Kuliko Wewe. Kwako Yupo Tu Kwa Sababu Fulani, Unapomlazimisha Kumuoa Au Kuishi Naye, Ni Kama Unajitengenezea Tu Bomu Ambalo Litakuja Kulipuka Hapo Baadaye.
Matatizo Ya Kwenye Ndoa Nyingi Kwa Sasa, Yanaanza Na Suala La Watu Kuoana Ikiwa Mmoja Wapo Hampendi Mwenzake. Yaani Mwanamke Ameingia Kwenye Ndoa Lakini Hampendi Mwanaume Aliyemuoa. Anaye Mwingine Tofauti Kabisa Ambaye Ndiye Anampenda Kwa Dhati.
Mwanamke Wa Aina Hii, Hata Kama Atakuwa Mke Wako Hesabu Tu Maumivu Huko Baadaye. Atakufanyia Visa Ili Mradi Tu Na Mwisho Wa Siku Mtaishia Kuachana Maana Hutaweza Kuvivumilia. Ndiyo Maana Nasema, Ni Vizuri Sana Wanaume Wakatoa Nafasi Ya Wanawake Kuwa Sehemu Ya Maamuzi Katika Uhusiano.
Kuwaacha Wanawake Nao Watoe Uamuzi, Kutasaidia Sana Katika Mustakabali Wa Mahusiano Yenu. Mapenzi Ni Ya Watu Wawili, Kila Mmoja Aridhie Kwa Dhati Kuifanya Safari. Usimlazimishe Mwanamke Eti Kwa Kuwa Wewe Ni Mwanaume, Eti Kichwa Cha Familia, Nani Kasema?
Kuepuka Mateso Ya Mapezi, Ni Vizuri Sana Kujenga Utamaduni Huu. Umemuona Mwanamke, Umempenda Wewe Nadi Sera Zako Halafu Muache Naye Akufanyie Tathimini. Akijiridhisha Kama Anakupenda, Atakueleza Na Mtayafurahia Maisha Sababu Wewe Tayari Unampenda Na Yeye Amekupenda.
Akikukataa Pia Mshukuru Mungu, Maana Anaweza Kuwa Na Sababu Za Msingi. Muache Awe Huru Kufanya Maisha Yake Kuliko Kulazimisha Awe Wako Kwa Gharama Yoyote, Atakuja Kukuumiza Tu Bure!
Tukutane Wiki Ijayo Kwa Mada Nyingine Nzuri. Unaweza Kunifuata Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii; Instagram&Facebook: Erick Evarist, Twitter: Enangale.
Kama kuna ukweli fulani hivi hapa
ReplyDelete