Kwa Kwenye Ndoa tu: Hivi Kumkaribisha Rafiki Nyumbani ni Kosa?

Wakuu,

Nimeoa sasa nina mwaka mmoja. Imetokea kitu mke wangu kakasirika sana sa sijui ni kosa au sio kosa. Tunaishi Dar.

Kuna rafiki yangu ambae tulisoma nae primary na secondary pia chuo UDSM kaniomba kufikia kwangu kwa siku moja. Yeye anaishi Mwanza anakuja Dar kufanya presentation just a single day.

Mimi naishi nyumba ina room tatu, na niko mimi na mke wangu tu, nikaona haina haja hata kumtaarifu wife kuhusu jamaa kuja hapa home nikijua nikirudi home jioni ntamwambia kuwa leo tuna mgeni.

Jamani nashangaa nafika home tumekaa vizuri tu, sasa hivi namwambia Leo saa nne usiku tutampokea jamaa ambae pia amekua akisikia stories zake kwangu kama rafiki wa karibu sana. Lakini mke kaja juu eti hakuna mtu kuja hapa, eti lazima ningemuuliza yeye ili ajibu yes or no.

Mimi nimemwambia nilichukulia simple tu coz jamaa hakai hata siku 2 anarudi Mwanza. Lakini pia mimi pia huwa nikienda Mwanza nafikiaga kwake hata bila taarifa, huyu ni rafiki lakini ni kama ndugu.

Hapa amekasirika ile mbaya.

Je wanawake mko hivi au mliooa siku nyingi, je ni kosa hilo?

By Masabile/JF

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post