Mikono yetu ni kiungo muhimu sana kinachoweza kupapasa karibu asilimia
99 ya miili yetu bila shida, lakini tafiti zimeonesha kuwa ni hatari
zaidi kwa afya yetu kushika sehemu kadhaa hususan sehemu hizi tano.
Katika hali ya kushangaza, utafiti uliofanywa na jopo lililoongozwa na
Profesa Kelly Reynolds wa Chuo cha Zuckerman College of Public Health
kilichoko ndani ya Chuo Kikuu cha Arizona, unataja maeneo hayo ya mwili.
Baadhi ya maeneo hayo ni haya yafuatayo:
Macho
Kama jicho lako halikulazimishi kulishika labda pale unatoa uchafu wa
aina yoyote kwa namna inayofaa, hakikisha hauligusi kabisa. Hii ni kwa
sababu mikono yetu inabeba mambo bakteria ambao wanaweza kudhuru macho
yetu taratibu na kudhurika bila kufahamu haraka.
Uso
Uso ni sehemu ambayo ni rahisi sana kupeleka mkono mara kwa mara. Ni
ngumu sana kuacha kufanya hivyo hususan kwa tunaofanya kazi za kutoa
jasho au kutembea sehemu ambazo zinatoa jasho. Pamoja na mambo hayo,
wataalam wamebaini kuwa ngozi ya uso ni ngozi ya kipekee na inapaswa
kutunzwa kwa uangalifu zaidi. Mikono yetu ambayo hubeba mafuta mafuta
pamoja na bakteria inaweza kudhuru ngozi zetu za uso.
Mdomoni (Nje na Ndani)
Utafiti zilizofanywa hivi karibuni nchini Uingereza umebaini kuwa mtu
ambaye ameboreka (bored) kazini hushika maeneo ya mdomoni zaidi ya mara
23.6 kwa saa moj. Hali hii ni tatizo kubwa kwani utafiti umebaini kuwa
robo tatu ya bakteria wabaya hupitia kwenye mdomo.
Ndani ya Pua
Kuna watu ambao kuchokonoa mapua yao ni sehemu ya tabia iliyojengeka.
Kwa bahati mbaya, tafiti za kitabibu zimebaini kuwa watu wanaochokonoa
pua zao kwa vidole wako katika hatari kubwa zaidi ya kushambuliwa na
bakteria (staph bacteria) zaidi ya wale ambao hawafanyi hivyo.
Ngozi ya chini ya kucha
Ni kosa kubwa kutunza kucha zako kuwa ndefu kiafya. Kucha hubeba uchafu
hata ule ambao huwezi kuuona kwa macho, bakteria wanaweza kujificha
chini ya ngozi za kucha yako. Bakteria hao wanaweza kuwa chanzo kikubwa
cha kuharibu afya yako. Hivyo, jitahidi kutofuga kucha, hakikisha kucha
zako ni fupi kwa kiasi cha kutosha ili usiipe nafasi bakteria kuishi.
Lakini kama unafuga kama urembo, unapaswa kuwa na matunzo ya ziada ya namna ya kupambana na bakteria ambao huwaoni kwa macho.
Note: Sehemu za siri ni shemu ambazo kila unapotaka kuzigusa
fahamu kuwa ni sehemu ambazo zikiguswa na bakteria uliowasomba na mikono
yako zinaweza kukusababishia madhara makubwa.
Tags
Afya