January 22 2018 beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso amejikuta akiingia matatizoni baada ya kujikuta akikamatwa na Polisi kwa madai ya kumpiga shabiki na kuzimia baada ya mchezo wao dhidi ya Simba uliyomalizika kwa Simba kupata ushindi wa magoli 2-0.
Nyosso amekamatwa na Polisi kufuatia kosa hilo ambapo mashuhuda wanadai kuwa baada ya mchezo huo wachezaji wa Kagera Sugar wakielekea vyumba vya kubadilishia nguo walikuwa wakitolewa maneno makali na mashabiki uvumilivu ukamshinda Nyosso na kumpiga ngumi shabiki huyo na kupoteza fahamu.
Gari la wagonjwa lililazimika kumkimbiza hospitali shabiki huyo kwa ajili ya kuhakikisha anapatiwa matibabu, Mpemba Blog inaendelea kufuatilia kwa kina taarifa hizo.
Tags
Michezo