UKISIKIA ushoga umepamba moto, basi ni huu wa staa mwenye jina kubwa Bongo, Wema Sepetu na mwanamuziki wa kike wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ambapo Wema anasema shosti yake huyo ‘ameibeba roho yake’ hivyo akiibwaga amekwisha.
“Unajua hakuna kitu chenye raha kama umepata rafiki anayekupenda na kukujali mpaka moyo wako unakubali, kwa upande wangu kama kutekwa, nimetekwa mzimamzima, yaani nampemda kufa,” alisema Wema huku akiangua cheko kama lote.
STORI NA IMELDA MTEMA, GPL
Tags
WASANII