Jaydee Atoa Pole kwa Wasanii wa Kike Asema Wanaotoa Ngono Wanatoboa

Msanii  wa Muziki wa Bongo Flave, Judith wambura, maarufu kwa jina la Lady Jaydee ametoa pole kwa wasanii wa kike  kwa yote ambayo wanapitia.

“Poleni sana wasanii wa kike kwa yote mnayopitia, mnayoweza na msoweza kuyaongelea,” aliandika Jaydee katika ukurasa wake wa twitter

“Nasema tena pole sana. Sio rahisi kama inavyodhaniwa au kuonekana, mngekuwa wazazi labda ingewasaidia mimi huwa naropoka liwalo na liwe. Love toka kwa Dada mkuu,”


Jaydee amesema  ” Wanaoweza kutoa ngono wanatoboa wasioweza wanakata tamaa wanaachia njiani,”

Msanii huyo amesema hilo ni jibu la kwanini wasanii wa kike ni wachache kwenye tasnia.

“Sio kila mtu anaweza kutoa mwili wake tu popote,” aliandika Jaydee

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post