Nyota wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo, ametakiwa kukodisha akaunti yake ya mtandao wa Instagram kwa dau nono kwa muda wa mwaka mmoja.
Shirika kubwa la uwekezaji la Marekani lilimpigia simu nyota huyo na kumuahidia kumlipa donge nono la Euro milioni 100 awakodishe kwa kipindi cha mwaka mmoja ukurasa wake binafsi wa mtandao wa Instagram.
Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba Ronaldo aliwajibu kwamba atalifanyia tathmini pendekezo hilo.
Ronaldo ana wafuasi wapatao milioni 187 katika mtandao wa Instagram, aliingiza kiasi cha Paundi za Uingereza milioni 38.2 kutoka shirika hilo.
Cristiano Ronaldo ndiye nyota anayeingiza pesa nyingi kupitia akaunti yake ya Instagram, katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita katika post za Instagram 49 kwa wastani alilipwa kiasi cha Dola 975,000 kwa kila posti moja ambapo kwa mwaka mzima idadi inafikia Dola 47.8 Milioni (Takribani TShs Bilioni 109.8).
Toa maoni yako
Tags
MICHEZO KIMATAIFA