Hamissa Mobetto Adai Kuwa Kwenye Mahusiano ya Pande Mbili

Kwa wasanii wengi wa hapa nchini ukiwauliza kuhusu mahusiano yao watakujibu kwamba  yapo "private" yaani binafsi au mahusiano yao yapo "secrect" kwa maana yake ni ya siri.


Sasa EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na msanii Hamisa Mobetto ambaye amesema kwa sasa yupo kwenye mahusiano ya pande zote mbili kati ya hayo, pia ametueleza utofauti wa kuwa kwenye mahusiano binafsi na yale ya siri.

"Sasa hivi nipo kwenye mahusiano na mtu fulani hivi wa kushangaza yaani amazing, na mahusiano yangu yapo katika pande zote mbili yaani binafsi na siri sidhani kama yatakuja kuwa mbele za watu, tofauti ya kuwa private ni mnaamua wenyewe kuwa hivyo ila watu wanajua kabisa kwamba mpo kwenye mahusiano" amesema Mobetto

"Ila mahusiano ya siri ni yale ambayo mpo na mambo yenu binafsi na hakuna anayejua kama mpo kwenye mahusiano, ndiyo maana kwangu mimi nikasema mahusiano yangu yako katika pande zote mbili". ameongeza 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post