Msanii Killy ambaye amejitoa katika lebo ya Kings Music Records, amesema ameamua kuchukua uamuzi huo kutoka kwa mama yake kwa sababu ndiyo mtu pekee aliyekuwa akimsapoti na anamfuatilia mienendo yake.
Killy amesema hapendi kuchanganya kazi zake na familia ila inapotokea suala kama hilo inabidi amsikilize mzazi, kwa sababu mama yake ndiyo mtu aliyekuwa anampa nauli tangu zamani na anataka aone faida anazozipata popote anapokuwepo.
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Killy amesema "Suala la kutoka Kings Music lilianzia kwetu sisi kabla ya mtu yeyote kwa sababu tulikuwa na mambo yetu kichwani, japo mwanzo tulisema wazazi wetu ndiyo walichangia, Mama yangu ndiyo mtu ambaye alikuwa ananipa nauli tangu zamani, ananifuatilia mienendo yangu, popote nitakapokuwepo lazima ajue ninapata faida gani na kitu gani nafanya"
"Ila nilimwambia mama yangu anipe sababu tatu za mimi kutoka Kings Music ila yeye akanipa tano, alivyoniambia nikainamisha kichwa chini mimi mwenyewe nikashindwa hata cha kuongea" ameongeza.
Tags
WASANII