Zari Hassan Afunguka Makubwa 'Nilishawahi Kufanya Kazi ya U House Girl'

Mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan  kwa mara ya kwanza ametoa ufichuzi kuhusu jinsi alivyopitia maisha magumu hapo awali kabla ya umaarufu na   amafanio ambayo ameyapata kupitia shughuli zake nyingi .Kupitia ujumbe katika Instragram Zari  ,mama ya watoto watano amesimulia jinsi alivyowahi kufanya kazi ya nyumba nchini Uingereza  ili kujikimu kimaisha .

Zari ameandika haya kupitia Instagram yake:

 LIFE LESSONS Life can be a rollercoaster and you will never know where you'll end up. From studying my cosmetology course in th UK ( which hasnt helped me) while doing house girl work to pay my accommodation (yes ive been a maid before)to running through buses to get to my next stop woodgreen where i worked as a cashier and sometimes as an isle packer in sainsbury. Friend, i started out early wasnt even sure why me. But the inner voice in me wanted better. My dad had left, my mom was doing tailor jobs day and night i couldnt stand seeing her struggle. I couldn't stand her pain. I was living with my aunt in the uk who treated me like a step child. Gooosh🙄 Been through boutiques, long economy flights to china in between building a school and having babies. My music and tv career is a story for another day. Phew😪 All I'm saying, consistency is key. Doesnt matter where you are or what you do. Just do it.


Zari ameelezea kujitolea kwake kufanya kazi za hapa na pale huku akiendelea  na masomo yake ili kuboresha maisha yake na familia yao hasa baada ya babake mzazi kuondoka na mamake akifanya kazi kama mshonaji .

‘Nilisikitika sana kumwona mamangu akiteseka kila uchao’ amesema Zari katika ujumbe huo mrefu ambao pia umevutia hisia mbali mbali za mashabiki wake ambao wamesifia ujasiri wake . Akiwa Uingereza ,Zari amesema alikuwa akiishi na shangazi yake ambaye alimchukulia kama mtoto wa kambo ,hali inayoonyesha huenda alipitia mateso . Lakini ukakamavu wake na bidii vimemfikisha alipo sasa na ujumbe wake amesema unalenga kuwapa watu zaidi ari ya kutaka kufaulu maishani .

Photo Credits: Hisani

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post