Watu Maarufu Marekani Wenye Majina ya Kiswahili...

Kwa mujibu wa gazeti la Omaha World-Herald tangu miaka ya 1960, wazazi wengi wa Marekani wenye asili ya Afrika wamekuwa wakiyageuza maneno ya Kiswahili kuwa majina na kuwapa watoto wao

Baadhi ya majina ya watu au makundi maarufu ambayo yana Kiswahili ni Taraji Penda Henson ambaye ni muigizaji wa Tamthilia maarufu ya Empire

Sanaa Lathan, mnenguaji na mwigizaji. Ameigiza kwenye filamu kama vile American Assassin (2017) n.k. Talib Kweli Green, Mwanamuziki huyu wa Hip Hop. Maana halisi ya jina lake ni Mtafuta Ukweli, mmoja kati ya watoto wake amemuita Amani

Zuri Hall, mtangazaji wa televisheni nchini Marekani. Wale wapenzi wa burudani, urembo na udaku watakuwa wamewahi kumuona kupitia E! News, The Challenge ya MTV

Amani Askari Toomer, alikuwa mchezaji wa American Football. Black Uhuru, kikundi cha muziki wa 'reggae' kilichoundwa nchini Jamaica mnamo 1972. Ras Jua Baraka ni Meya wa 40 wa sasa wa Newark, New Jersey

Amiri Baraka, baba wa Ras Jua Baraka. Alikuwa ni mwanazuoni na mwandishi wa vitabu vingi vya ushairi na alifundisha katika vyuo vikuu kadhaa. Rehema Ellis huyu ni mwandishi wa habari wa TV nchini Marekani

Je, Watu gani wengine maarufu unaowafahamu wenye majina ya Kiswahili kutoka sehemu wasipozungumza Kiswahili?

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post