Ujerumani
itaondoa baadhi ya wanajeshi wake waliowekwa kama sehemu ya muungano
unaopambana dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, nchini
Iraq, wizara ya ulinzi imesema leo, katika hatua ya kutoridhishwa na
shambulio la Marekani la ndege isiyokuwa na rubani ambalo limemuuwa
jenerali wa ngazi ya juu wa Iran.
Kiasi cha wanajeshi 30 waliowekwa mjini Baghdad na Taji
wataondolewa na kupelekwa nchini Jordan na Kuwait, msemaji wa wizara ya
ulinzi ameliambia shirika la habari la AFP, na kuongeza kwamba
kuondolewa huko kutaanza hivi karibuni.
Shirika
la habari la Ujerumani, dpa, limesema Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani
Annegret Kramp-Karrenbauer na Waziri wa Mambo ya Kigeni Heiko Maas
wamewaandikia wabunge kuwa wanajeshi walioko katika vituo mjini Baghdad
na Taji nchini Iraq wataondolewa kwa muda.
Mawaziri
hao wawili wamesisitiza kuwa mazungumzo na serikali ya Iraq kuhusu
kuendelea na kikosi cha kutoa mafunzo kwa vikosi vya Iraq yataendelea.
Tags
Kimataifa

Hii balaa
ReplyDelete