Sheikh Kipozeo ampa neno Stamina "Ukiona mwanamke anakuvunjia heshima tafuta mwingine"

Hilal Shaweji maarufu kama Sheikh Kipozeo, amemshauri msanii wa HipHop Stamina juu ya kukimbiwa na mkewe na kumsihi atafute mwanamke mwingine kama amevunjiwa heshima ndani ya ndoa yake


Sheikh Kipozeo ameeleza hayo wakati akipiga stori na  show ya Planet Bongo ambapo amesema wanawake wapo wengi na mungu amewaleta wawe wengi kuliko wanaume.

"Mimi namuhusia tu kwamba wanawake wapo wengi, kwahiyo ukiona mwanamke anakuvunjia heshima unatafuta mwingine tu, japokuwa yule aliyepita si kama wa huyu atakayempata sasa hivi, lakini utamzoea tu na atakuwa kama yule, sio jambo la kusikitika sana ndiyo maana Mungu amewaleta wanawake wengi duniani kuliko wanaume" amesema Sheikh Kipozeo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post