JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa wanahitaji kupata ushindi leo mbele ya Leicester City kwenye mchezo wao ambao ni wa Ligi Kuu England.
Liverpool ni vinara wa Ligi Kuu England wakiwa nafasi ya kwanza na pointi 49 watamenyana na Leicester City iliyo nafasi ya pili na ina ponti 39.
'Ni sawa kwetu kutafuta ushindi kama ilivyo kwenye mechi nyingine ambazo tumecheza ndani ya Ligi Kuu England, Ikiwa unatafuta mafanikio na unakutana na ushindani ni lazima uendelee kupambana ili uyavute hayo mafanikio karibu zaidi.
'Hatuna hofu yoyote ile kwa sasa zaidi ya kutazama nini ambacho tunakitaka kwa ajili ya maisha yetu hapo baadaye ila tutadhihirisha hiki kwenye siku ya Boxing day," amesema.
Msimu uliopita wa mwaka 2018-19 Liverpool ilimaliza Ligi Kuu England ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 97 ilishinda mechi 30 ilipoteza mechi moja mbele ya mabingwa watetezi Manchester City na ililazimisha sare saba.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA