Waliokuwa Makocha wa Simba Watajwa Kutua KMC


Baada ya uongozi wa klabu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC, kutoa taarrifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na kuachana na aliyekuwa kocha wao Jackson Mayanja kutokana na kutoridhishwa na maendeleo ya timu hiyo tangu mwanzoni mwamsimu huu, imeripotiwa baadhi ya makocha wapo katika mpango wa kujiunga na kikosi hicho kwaajili ya kukinoa.

Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya KMC upo kwenye mazungumzo na makocha Masoud Djuma pamoja na Joseph Omogo waliowahi kuinoa Simba.

 Omog ambaye ni raia wa Cameroon, anatajwa kuchukua nafasi ya Mayanja sambamba na Masoud ambaye ni raia wa Burundi.

 Kuna uwezekano makocha hao wawili wanaweza kuwa sehemu ya timu ya KMC na muda wowote kuanzia sasa wanaweza wakatangazwa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post