Shomari Kapombe atoboa siri ya kutoka mshambuliaji hadi beki

Shomari Kapombe atoboa siri ya kutoka mshambuliaji hadi beki
Mchezaji wa Simba, Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wachache wanaoweza kucheza nafasi nyingi uwanjani na kutekeleza majukumu ipasavyo.

Kwa sasa anacheza sana eneo la ulinzi (kulia) lakini anauwezo mkubwa wa kusaidia kushambilia akitokea pembeni-kulia. Anaweza pia kucheza kama beki wa katikati na kiungo wa kati na amewahi kucheza mara kadhaa.

"Nilianza maisha ya soka kama mchezaji wa nafasi za mbele, nikiwa timu ya U14 nilikuwa nacheza kama mshambuliaji mpaka nakwenda U17 bado nilikuwa nacheza nafasi ya ushambuliaji." anaeleza Kapombe.

Anaendelea kwa kusema, "Kuna mchezaji mmoja (alikuwa nahodha wetu) aliondoka kwa hiyo kocha akaanza kujaribu kunivuta nicheze eneo la kiungo. Mazoezi yalikuwa yanaanza saa 9 kocha akawa ananiambia nifike uwanjani saa 8 nilikuwa nafika saa 8 ananifundisha na vitu vingine ananiandikia, vitu hivyo hadi leo vinanisaidia."

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post