SIMBA INADAIWA MABAO HAYA NA YANGA ILI KUCHUKUA UBINGWA



WASHAMBULIAJI wa Simba ambao wanaunda safu ya ushambuliaji yenye mabao mengi mpaka sasa, wanadaiwa mabao 6 tu kuvunja rekodi iliyowekwa na ile pacha ya Yanga msimu wa mwaka 2015/16.
Msimu wa 2015/16 safu ya ushambuliaji ya Yanga iliyokuwa inaundwa na Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Simon msuva wao walifunga jumla ya mabao 47.
Tayari safu ya Simba inayoongozwa na Kagere imeshafunga jumla ya mabao 41 tofauti ya mabao sita tu kuvunja rekodi iliyowekwa na safu ya Yanga ambayo mpaka sasa haijawahi kufikiwa na pacha yoyote bongo.
Simba wamebakiwa na michezo nane kukamilisha Ligi Kuu Bara, hivyo kama watatumia nafasi zao vizuri huenda wakaifikia rekodi hii.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post