AISHI MANULA ANAPATA TAABU SANA KANDA YA ZIWA



MLINDA mlango namba moja wa mabingwa watetezi wa ligi Simba, Aishi Manula anapata taabu sana akiwa kanda ya ziwa kutokana na kuruhusu nyavu zake kutingishwa ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza na kupoteza pointi sita muhimu.

Manula ambaye mpaka sasa amedaka mechi 24 kati ya mechi 26 na kuruhusu kufungwa mabao 10 alianza kupoteza mbele ya Mbao mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa uwanja wa CCM kirumba kwa kufungwa bao 1-0.

Pia mchezo mwingine uliochezwa kanda ya ziwa dhidi ya Kagera Sugar Manula alikubali kuruhusu nyavu zake kutingishwa mara mbili ikiwa ni idadi kubwa ya mabao ambayo amefungwa kwa msimu huu akiwa langoni na Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 uwanja wa Kaitaba.

Rekodi zinaonyesha kwamba kama Manula akianza kutingishwa kipindi cha kwanza michezo ya kanda ya ziwa imekuwa ni ngumu kwa Simba kushinda licha ya juhudi za wachezaji kupambana hazifui dafu.

Ni mchezo mmoja tu ambao Simba walifanikiwa kupindua matokeo kibabe nao haikuwa kanda ya ziwa ulikuwa dhidi ya Tanga uliochezwa uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Simba ilianza kufungwa kipindi cha kwanza ila kipindi cha pili walipindua na kushinda kwa mabao 2-1.

Mabao mengine aliyofungwa Manula ilikuwa dhidi ya Alliance FC Simba 5-1, Mwadui 1-3 Simba, African Lyon 1-2 Simba, Azam 1-3 Simba, Coastal Unon 1-2 Simba, Lipuli 1-3 Simba na KMC 1-2 Simba.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post