''Tutakuwa tofauti kidogo'' - Yanga


Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa timu yake imefanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo wa ligi kuu kesho dhidi ya KMC na wamefanya maandalizi mazuri yenye utofauti kutokana na aina ya timu wanayokutana nayo.

Kocha huyo raia wa DR Congo ameweka wazi kuwa KMC ni timu iliyopanda daraja msimu huu lakini ina wachezaji wazoefu hivyo hawawezi kuwabeza ndio maana wamejianda kwa kuzingatia aina ya mechi.
"Tumejiandaa vyema kama ambavyo huwa tunajiandaa michezo mingine kikubwa ni kwamba tutaingia uwanjani na kucheza kwa aina ya tofauti kidogo kutokana na timu ambayo tunacheza nayo, KMC ni timu iliyopanda ligi kuu msimu huu ila siwezi kuwabeza maana wana mwalimu mzoefu na wachezaji wazuri na wazoefu pia'', amesema Zahera.
Yanga kwasasa ina alama 19 katika mechi 7 ilizocheza msimu huu ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya Azam FC ambao ni vinara wa ligi wakiwa na alama 24 baada ya leo kushinda mechi yao dhidi ya JKT Tanzania.
Kwa upande wa KMC yenyewe ipo katika nafasi ya 12 ikiwa na alama 10 kwenye mechi 10 ilizocheza msimu huu.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post