Ibrahim Ajibu aipa pigo Yanga

Klabu ya soka ya Yanga imethibitisha kumkosa nyota wake, Ibrahim Ajibu ambaye amepata maumivu ya mgongo kwenye mazoezi wakati timu yake ikijiwinda na mchezo wa leo dhidi ya KMC.



Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa Ajibu hatacheza mchezo wa leo dhidi ya KMC na bado haijulikani lini atarejea lakini yupo kwenye matibabu.
''Ibrahim Ajibu hatokuwa sehemu ya mchezo wa Yanga dhidi ya KMC, baada ya kupata maumivu ya mgongo. Kwasasa anaendelea na matibabu'', imeeleza taarifa ya Yanga.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa nyota huyo ambaye yupo kwenye kiwango bora kwasasa anapata matibabu chini ya uangalizi wa daktari wa timu hiyo Edward Bavu na wanaamini atapona haraka na kurejea kwenye majukumu
yake.
Msimu huu tayari Ajibu ameshafunga mabao 3 na kusaidi mengine 7 hivyo kuisaidia timu yake kufikisha alama 19 katika mechi 7 ikiwa katika nafasi ya 3.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post