TP Mazembe, Casablanca, kuweka rekodi Super Cup Afrika


Leo Jumamosi Februari 24, 2018, utachezwa mchezo wa Super Cup Ukiashiria kufunguliwa rasmi kwa msimu wa kimashindano wa michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho Afrika, mabingwa wa Caf Champions Leagu msimu uliopita Wydad Casablanca dhidi ya TP Mazembe ambao ni mabingwa wa Caf Confederation Cup.

Hii ni Super Cup ya 26 tangu kuanza kwa mchezo huu maalum ambao unafungua michuano ya kimataifa kwa ngazi za vilabu barani Afrika lakini kuelekea katika mchezo huo kati ya Wydad Casablanca dhidi ya TP Mazembe ni kwamba timu zote mbili zina historia ya kucheza Super Cup barani Afrika.

Wydad Casablanca wameshacheza mara mbili (1993 na 2003) lakini mara zote waliambulia patupu, kwa upande wa TP Mazembe, wenyewe wamecheza Super Cup mara nne (2010, 2011, 2016 na 2017) Mazembe wanaonekana kuwa wababe katika Super Cup kwa sababu wameshinda taji hilo mara tatu.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa kwenye kongamano maalu la Fifa nchini Tanzania ni pamopja na Video Assistance Referee (VAR) ambayo imeshaanza kutumika katika maeneo mengine duniani na imekuwa na mijadala mingi.

Wakati inaanzishwa VAR ilikuwa na lengo la kuwasaidia waamuzi katika kufanya maamuzi sahihi lakini wakati mwingine wanasema VAR imekuwa ikiwapotosha waamuzi na kuwakera watazamaji. Mfano mzuri wa hivi karibuni ni mechi kati ya Huddersfield Town dhidi ya Manchester United ambapo goli la Juan Mata lilikataliwa na VAR haikuwa msaada kwa waamuzi wa mchezo huo.

Kuelekea katika mchezo huo, Wydad Casablanca hawafanyi vizuri katika ligi yao ya ndani nchini Morocco, wanashika nafasi ya 10 kwenye msimamo na mwezi Januari walimfukuza kocha wao Hussein Ammoutta ambaye aliwapa ubingwa wa Caf Champions League nafasi yake imechukuliwa na Faouzi Benzarti moja kati ya makocha wenye historia nzuri barani Afrika lakini kuna mabadiliko makubwa sana katika timu ya Wydad Casablanca kwa sababu baadhi ya wachezaji waliokuwanao msimu uliopita wameshaondoka.

Kwa upande wa TP Mazembe chini ya kocha wao Pamphile Mihayo wenyewe watamkosa kiungo wao Nathan Sinkala kutokana na majeraha.

Bingwa wa mchezo wa Super Cup atachukua kiasi cha dola 100,000 za kimarekani, mshindi wa pili atapata dola 75,000.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post