BREAKING NEWS: MO APATIKANA AKIWA HAI, ANENA HAYA

Mfanyabiashara Maarufu hapa Nchin Mohammed Dewji amepatikana akiwa hai leo Alfajiri baada ya kutekwa na watu wasiojulikana tangu 11/10/2018.

Kwa taarifa Zaidi tutaendelea kukuletea muda sio mrefu.

Akizungumza na East Africa Television LTD baba Mzazi wa Mohamed Dewji ,  Mzee Gulam Hussein amethibitisha mwanaye kupatikana na kurudi nyumbani salama
Pia 'personal Assistant ' (PA) wa Mohammed Dewji Barbara Gonzale ameithibitishia EATV kuwa amepatikana na kuzungumza maneno yafuatayo;
“Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama.” — Mohammed Dewji 
Wakati huo huo Waziri January Makamba amesema amefika nyumbani Mo Dewji na kumuona kisha akaandika;
"Nimemuona na kuongea kwa kirefu na Mohammed Dewji. Ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni. Mnamo saa nane usiku, watekaji waliamua kumtupa kwenye maeneo ya viwanja vya Gymkana. Naamini Polisi watatoa taarifa za ziada kuhusu kilichojiri.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, amesema, 
 "Mo Dewji amepatikana akiwa mzima wa afya, baada ya kumhoji anasema alivyotekwa pale Collesium gari ilitembea kwa speed kama dakika 15 na kuwekwa mahali kama kwenye chumba".

Tazama video
Kamanda Mambosasa na Mo Dewji wakizungumzo



Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post