Kiungo mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajibu, alikuwa ndani ya kikosi kilichoifunga mabao 3-0 Alliance School na anaongoza kutoa pasi za mabao ameshatoa pasi 8 amesema kuwa kinachomfanya awe katika ubora ni ushirikiano anaopata ndani ya timu.
Ajibu amekuwa akifanya vizuri msimu huu ambapo mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao 3 na kuahidi kuwa hatarajii kupunguza kasi yake.
"Ligi ni ngumu na kila timu imejipanga vizuri,kikubwa ambacho kinasaidia ni ushirikiano ndani ya timu,maelekezo kutoka kwa mwalimu yananijenga kila siku.
"Namshukuru Mungu kwa kuwa nafanya kazi kwa ajili ya timu, bado nitaendelea kupambana kwani kuna michezo mingi ambayo inafuata ,mashabiki waendelee kutupa sapoti"alisema.