AJIBU AWAPIGA MKWARA HUU SIMBA

Image result for ajib yanga


Wakati kikosi cha Yanga, kikiendelea kujifua mara mbili kwa siku huku Morogoro, kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu amewataka mashabiki kutulia na kutokuwa na hofu yoyote.

Simba na Yanga zitapambana Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wenye ushindani mkubwa.

Kwa mujibu wa Championi Jumatano, Ajibu ambaye anaongoza kwa kutengeneza nafasi za kufunga ndani ya Yanga lakini pia ligi kuu msimu huu amesema kuwa moto walioanza nao katika mechi za timu hiyo zilizopita ndiyo watakaoendelea nao dhidi ya Simba.

“Binafsi nimejipanga kwa ajili ya mchezo huo na ni matumaini yangu kuwa tutafanya vizuri kama ambayo tumekuwa tukifanya katika mechi zilizopita.

“Niwaombe tu mashabiki wetu kutokuwa na hofu yoyote juu ya mchezo huo na wauchukulie kama walivyokuwa wakichukulia mechi zetu nyingine zilizopita lakini pia wasisahau kutuombea kwa kila hatua tunayopiga,” alisema Ajibu.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post