JIPYA LAIBUKA HUKO LIVERPOOL KUHUSIANA NA KIPA WAKE KARIUS


Kama ulikuwa unadhani kipa wa Liverpool, Loris Karius atapipigwa benchi ama kuondoshwa klabu hapo basi si hivyo unavyofikiria.

Ripoti kutoka vyanzo mbalimbali barani Ulaya vimeeleza kuwa uongozi wa juu kutoka kwa majogoo hao wa Anfield umefunguka na kusema ataendelea kuwa namba moja msimu ujao.

Karius ambaye anakumbukwa kwa kufungwa mabao matatu katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Liverpool ilipokutana na Real Madrid, ametajwa kuendelea kucheza nafasi hiyo.

Baada ya kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Madrid, Karius alipewa lawama nyingi kutoka kwa mashabiki na baadhi ya wadau wa soka kutokana na zile bao mbili alizofungwa na Gareth Bale.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post