ACHANA NA MAKAMBO, YANGA KUSHUSHA BEKI HUYU HATARI KUTOKA MOTEMA PEMBE


Achana na yule straika aliyetua Dar kwa ajili ya majaribio na klabu ya Yanga, imeelezwa pia mabingwa hao wa kihistoria nchini wanatarajiwa kushusha mwingine kutoka DC Motema Pembe FC ya Congo.

Baada ya Makambo kufuzu majaribio hapo Jangwani na sasa akisubiria kupewa mkataba ili awe mchezaji rasmi wa kikosi hicho, mabosi wa klabu hiyo wameanza mazungumzo na beki Yannick Litombo kuja kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi.

Harakati hizo za Yanga kuboresha kikosi chake zinafanywa kulingana na uwepo wa timu hiyo kwenye mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo hivi sasa inajiandaa kucheza mechi ya mkondo wa kwanza.

Yanga itakuwa ina kibarua Julai 18 jijini Nairobi dhidi ya mabingwa wa Ligi ya Kenya, Gor Mahia FC ambao hivi sasa wapo nchini Tanzania kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Kagame yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Tayari Yanga imeshapitisha baadhi ya wachezaji ambao wamefuzu majaribio ikiwemo mkongwe Mrisho Khalfan Ngassa pamoja na Makambo wa Motema Pembe.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post