Huko yanga hawana fedha za kusajili wachezaji lakini zoezi linaendelea kama kawaida!
Leo, mmoja wa wachezaji waandamizi wa Yanga aliyekuwa akihusishwa na vilabu vya Azam FC na Simba, amesaini kandarasi ya kuendelea kubaki Jangwani!
Mfumo aliokuja nao Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten wa kutoa taarifa za usajili bila ya kuweka wazi aliyesajiliwa umekuwa muafaka sana nyakati hizi.
Kwa kuwa baadhi ya timu zimeonyesha uwezo mdogo wa 'ku-scout' wachezaji wazuri, zinasubiri Yanga itangaze inamsajili nani ili ziwahi, mfumo huu sasa ndio kiboko yao.
Wengine wametishia kusajili wachezaji wote muhimu wa Yanga, lakini mpaka sasa hakuna aliyefanikiwa!
Muhimu ni kwa mashabiki wa Yanga kuwa na subira tu, waamini viongozi wao wako makini na zoezi zima la usajili.