Kwa mara ya kwanza katika historia June 2 2018 ndio tutaona mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup fainali kwa pasipokuzikutanisha moja kati ya Simba na Yanga huu ukiwa ni msimu wake wa tatu.
Kesho June 2 mchezo huo utachezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kwa kuzikutanusha timu Singida United dhidi ya Mtibwa Sugar, mvuto wa mchezo wa fainali hii hautokani na zawadi ya Bingwa kupewa Tsh milioni 50 bali kupata tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu wa 2018/2019.
Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao leo amejibu swali kuhusiana na kudaiwa kuwa Mtibwa Sugara hata akishinda hatoshiriki michuano hiyo kutokana na kufungiwa, Kidao ameeleza kuwa mshindi wa game hiyo ndio atakayeshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na sio vinginevyo.