Wafahamu binadamu wa ajabu wanaoishi baharini kama Vyura





WATU wa kabila la Bajau wanaoishi katika visiwa vya Malay, Mashariki ya Mbali, hutumia muda mwingi wa maisha yao baharini kama wanyama aina ya amfibia ambapo huishi katika mitumbwi au vibanda vilivyojengwa juu ya nguzo maalum au juu ya miamba iliyo karibu na bahari.
Isitoshe, watu hao huhama kila mara katika makundi na koo za nzima. Kuhusu chakula chao, kabila hilo huishi kwa kula chakula cha baharini tu. Katika kutafuta chakula hicho, inabidi watumia asiliia 60 ya muda wao wa kila siku wakiwa chini ya maji. Hili ndilo huwafanya wawe na uwezo wa ajabu wa kukaa chini ya maji kwa muda mrefu zaidi.
Kuna wakati wanaweza kuingia majini umbali wa mita zaidi ya 70 na kukaa huo kwa dakika tano, Katika zoezi hilo huwa wanabeba vitu vyenye kuwaongezea uzito ili kupunguza nguvu ya kuwarudisha juu ya maji. Vilevile huwa wanavaa miwani ya mbao yenye vioo maalum vilivyotengenezwa kutokana na mabaki ya vioo ambavyo haviwezi kuingiza maji
Kwa vile wato hao wameishi maisha hayo kwa muda mrefu (ushahidi wa kihistoria ukionyesha kwamba ni zaidi ya miaka 1,000), watafiti wengi wanasema kwamba watu hao wana vinasaba ambavyo vinawawezesha kuishi maisha hayo.Hili limethibitishwa na wataalam mbalimbali, wakiwemo wa Chuo Kikuu cha California, Marekani, hiyo ndiyo sababu inayowafanya kuingia katika maji baridi na kuweza kushikilia pumzi kwa muda mrefu bila kuwa na tatizo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post