Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kujitoa muhanga wa maisha yake kwa kile alichokieleza kuwa haogopi kuonekana mbaya kwa binadamu wa aina yoyote katika hii dunia kadri siku zinavyozidi kusonga mbele.
Kauli hiyo ya Shamsa Ford imekuja baada ya kuwepo wimbi kubwa la vijana wengi wa kizazi cha sasa kuhofia kufanya mambo yao ya kimaendeleo kwa kuhofia au kuogopa walimwengu kwa maneno yao yasiyokuwa na baraka hata wawafanyia jambo gani kubwa lakini mwisho wa siku wao wanaambulia kudharauliwa na mengineyo.
"Siku zinavyozidi kwenda nimejikuta siogopi kuonekana mbaya kwa binadamu yoyote. Nimegundua binadamu hata uwe mwema kiasi gani lazima atakutafutia kasoro ya kukutia ubaya", amesema Shamsa.
Pamoja na hayo, Shamsa Ford ameendelea kwa kusema "binadamu hata uwe mpole, mnyenyekevu na mwenye upendo lazima wakusengenye kwa ubaya ni ngumu sana kuishi na binadamu na huwezi kumlizisha kila binadamu ni bora uishi maisha unayoona wewe ni sahihi kwako".
Kwa upande mwingine, Shamsa Ford amesisitiza kuwa kuishi na binadamu kuna hitaji umakini wa hali ya juu pamoja na hekima ili mradi uende nae sawa bila ya kukwazana kwa namna yoyote ile.