Akiongea kwenye mahojiano maalum baada ya sherehe za utoaji wa tuzo za klabu hiyo ziizofanyika jana usiku, Manara ameweka wazi kuwa mkataba wa Pierre Lechantre unamalizika Juni 18 na haoni nafasi yake tena ndani ya Simba.
''Kocha Pierre kafanya kazi kubwa lakini sioni namna ya yeye kuendelea kubaki Simba baada ya mkataba wake kumalizika Juni 18, hivyo sina uhakika kama ataendelea na klabu labda asilimia 10 tu za kubaki hicho ndicho ninachofahamu mimi'', amesema.
Manara ameongeza kuwa maamuzi ya mrithi wa Lechantre yatafanywa na Kamati ya utendaji ya klabu chini ya Kaimu Rais Salim Abdallah. Lechantre mwenyewe alisikika akitoa kauli ya kuiaga klabu hiyo wakati akipokea tuzo ya benchi la ufundi usiku wa jana.
Kwa upande wa mashabiki wa timu hiyo kupitia maoni yao mitandaoni wameonekana kumpigia chapuo nguli wa timu hiyo Selemani Matola ambaye ni kocha wa Lipuli FC kuungana na kocha Masoud Djuma kwaajili ya kuinoa Simba.
Tags
SIMBA