Kombe la Dunia mwaka 2018: Mambo saba unahitaji kufahamu


Picha ya Kombe la Dunia
Kikosi cha Ujerumani ni kizuri kwa Penalti? Kucheza nyumbani kunasaidia kwa kiwango kipi? na ni mlinzi yupi wa Mexico aliye na rekodi sawa ya kufunga mabao na Cristiano Ronaldo?
Wakati Kombe la Dunia linaanza tunajibu hayo yote na mengine mengi.


1. Nani ameshinda Kombe la Dunia?
Brazil ndio wameshinda vikombe vingi zaidi vya Dunia. Kombe la mwisho lilikuwa mwaka 2002. Waliandaa kombe hilo mwaka 2014 lakini wakafungwa mabao 7-1 wakati wa nusu fainali na Ujerumani.

Nani ameshinda Kombe la Dunia mara nyingi zaidi
Hakuna nchi nje ya Ulaya au Amerika Kusini imeshinda Kombe la Dunia, na ushindi kwa Ujerumani, Uhispania na Italia katika fainali za mwisho tatu unamaanisha kuwa ulaya inaongoza na vikombe 11 kwa 9 vya Amerika Kusini.
2. Nani amefunga mabao mengi zaidi?
Mfungaji mabao mjerumani Miroslav Klose anaongoza kwa kufunga mabao 16 kwenye mashindano manne ya Kombe la Dunia. Alistaafu mwaka 2016.
MBrazil Ronaldo ni wa pili kwa mabao 15, 8 kati yao akiyafunga wakati wa kombe la Dunia la mwaka 2002.
Wafungaji bora kombe la Dunia
Mfaransa Fontaine anaweka rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye Kombe moja la Dunia. Alifunga mabao 13 kwenye mechi sita wakati wa mashindano ya mwaka 1958.
3. Vipi kuhusu wachezaji wa sasa?
Kati ya wachezaji ambao wamefunga mabao 10 au zaidi wakati wa kombe la Dunia, ni Mjerumani Thomas Muller tu ambaye ataenda Urusi kama mchezaji.
Kujiunga na mwenzake Klose katika orodha hiyo, Muller atahitaji kufunga mabao matano kwenye Kombe la sasa la Dunia.
Mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez alishinda viatu vya dhahabu Kombe la Dunia lililolipita.
Wafunga mabao mengi watakaocheza Urusi
Rafael Marquez, mlinzi wa pekee aliye kwenye orodha atacheza kombe la dunia la tano kwa Mexico akiwa na rekodi sawa ya kufunga na ya Cristiano Ronaldo.
4. Timu hazipigi mikwaju jinsi zilikuwa zikifanya hapo awali.
Kombe la Dunia lililopita lilikuwa na mikwaju michache zaidi tangu mwaka 1966.
Licha ya hilo kulikuwa na takriban mabao 2.7 kwa kila mechi ikiwa ndiyo ya juu zaidi tangu Uhispania mwaka 1982.
Yaonakana kuwepo upungufu wa mikwaju ya masafa marefu
Makombora ya kulenga goli fainali kombe la Dunia
5. England inaweza kuwa na wakati mgumu lakini bado Ligi ya Primia inatawala
Tangu ipate ushindi mwaka 1966, England imepita robo fanali mara moja tu. Lakini hilo halijazuia nchi zingine kujaza vikosi vyao na wachezaji kutoka ligi za Uingereza.
Kuna wachezaji 130 wanaocheza Kombe la Dunia kutoka ligi kuu tatu za Uingerza ikilinganishwa na 81 kutoka Uhispania na 67 kutoka Ujerumani.
Wachezaji nyota wa ligi za nyumbani
6. Nchi mwandalizi hufanya vipi?
Hakuna mtu nchini Brazil atahitaji kukumbuka nyakati waliandaa Kombe la Dunia. Walipoteza kwa Uruguay mwaka 1950 na kwa Ujerumani kwa mabao 7-1 mwaka 2014.
Lakini nchi zingine hufanya vyema zinapoandaa Kombe la Dunia kutokana na uungwaji mkono wa nyumbani. Urusi watakuwa na matumaini ya kufuzu kutoka kwa kundi la Uruguay, Misri na Saudi Arabia
Ikiwa watafanikiwa Afrika Kusini itabaki nchi ya kwanza iliyoandaa Kombe la dunia kuweza kundolewa kwenye makundi.
Timu ya nyumbani mara nyingi hupata alama nyingi
7. Penalti
Hakuna mashindano ya Kombe la Dunia yamemalizika bila ya kupigwa penalti.
Ni mjerumani mmoja tu ambaye amekosa penalti ya Kombe la Dunia na wameshinda penalti zote ambazo wameshiriki.
Na la kushangaza England ndio wamefanya vibaya zaidi katika penalti katika historia ya Kombe la Dunia kwa kupoteza bila ya kushinda lolote.
Italia iliondolewa kwa njia mbaya zaidi mara tatu ikiwemo wakati wa mechi za mwaka 1994 wakati Roberto Baggio alipoteza penalti.
Nani ameshinda mechi nyingi zaidi kupitia penalti

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post