Kerr akizungumza mjini Nakuru Kenya, kwamba aliamua kuondoka Simba kutokana na matatizo lukuki yaliyosababishwa na viongozi anaweza kurejea na kuifundisha Simba ikiwa kama rundo la viongozi waliopo sasa wataondolewa.
“Bado baadhi yao wapo, ni watu ambao wanaingilia kazi za makocha, hawajui wanalolifanya na hakuna kocha anayeweza kuja akafanikiwa, lakini ni lazima uongozi wa sasa kama ni wamiliki, wawaondoe watu hao”, amesema Kerr.
Kerr ambaye alitimuliwa Simba kutokana na kuonekana kuwa hawezi kuipa mafanikio klabu hiyo, ameiwezesha Gor Mahia kuchukua ubingwa wa Kombe la SportPesa Super Cup kwa mara ya pili mfululizo, safari hii wakiifunga Simba kwa mabao 2-0 katika mechi ya fainali.