Kombe la Dunia: Vigezo vitakavyotumika timu kufuzu awamu ya muondoano


Argentina ya Lionel Messi nusura ibanduliwe lakini ushindi wa Nigeria dhidi ya Iceland ulifufua matumaini yao

Tunaelekea katika awamu wa mwisho ya mechi za makundi za Kombe la Dunia mwaka 2018.

Timu sita tayari zimefuzu lakini nafasi kumi bado zinang'ang'aniwa. Tazama ushauri wetu ili kuhakikisha kuwa timu zinaimarisha matumaini yao ya dimba hilo

Hivi ndivyo Fifa inagawana timu ambazo ziko na pointi sawa:

Orodha ya makundi kulingana na Fifa

1. Tofauti ya magoli.

2. Magoli yaliofungwa

Iwapo timu haziwezi kutofautishwa basi...

3. Mwenye idadi kubwa ya pointi katika kundi na mechi kati ya timu husika

4. Tofauti ya mabao kutokana na mechi za kimakundi kati ya timu husika

5. Idadi ya mabao iliofungwa katika mecho zote za kimakundi

Iwapo haitawezekana....

6. Idadi kubwa ya pointi zilizopatikana kutokana na mchezo wa timu husika kulingana na kadi za njano au nyekundu zilizopatikana katika mechi zote za kimakundi

Na hatimaye...

7. kupigiwa kura na kamati ya mipango ya Fifa

Group A

Image captionKundi AUrusi na Uruguay wamefuzu kutoka kundi lao. Urusi watafuzu kama washindi ikiwa watazuia kushindwa na Uruguay

Jumatatu 25 Juni

Saudi Arabia v Egypt, Volgograd Arena, 15:00 BST

Uruguayv Russia, Samara Arena, 15:00 BST

Mshindi anacheza na namba mbili Kundi B. Namba mbili kucheza na mshindi wa Kundi B.

Kundi B

KUNDI B

Mambo hapa yanazidi kuwa magumu.

Pointi moja ya Uhispania dhidi ya Morocco itawafanya kufuzu

Iwapo mabingwa hao wa Uhispania watapoteza watafuzu iwapo Ureno itaishinda Iran ama iwapo Ureno itafungwa mabao mengi na Iran ama iwapo mechi hiyo itakuwa na droo ya mabao machache na Uhispnia itapaoteza kwa zaidi ya bao moja.

Ureno itafuzu kupitia sare na Iran

Iwapo Ureno na Uhispania zitafungwa basi timu itakayopoteza kwa mabao mengi itaondoshwa .Iwapo zote mbili zitashinda basi basi timu yenye ushindi mkubwa itamaliza ya kwanza katika kundi B

Timu mbili bora kufikia sasa zina pointi sawa, tofauti sawa ya magoli na magoli yaliofungwa- zinaweza kutofautishwa na kadi nyekundu na njano zilizopata{ Uhispania ina kadi moja ya njano na Ureno ina kadi mbili).

Iwapo vigezo vyote hivyo viko sawa kutapigwa kura kuamua timu zitakazofuzu.

Iran itafuzu iwapo itapata ushindi dhidi ya Ureno, watashinda kundi hilo la sivyo Ureno nayo iibuke mshindi.

Jumatatu 25 Juni

Iran v Portugal, Mordovia Arena, 19:00 BST

Spain v Morocco, Kaliningrad Stadium, 19:00 BST

Mshinid kucheza na namba mbili Kundi A. Namba mbili kucheza na mshindi Kundi A.

Kundi C

Image captionKUNDI C

Ufaransa imefunzu katika raundi ya muondoano - pointi moja dhidi ya Denmark itawafanya kumaliza kama washindi wa kundi hilo.

Pointi moja dhidi ya Ufaransa itaifanya Denmark kufuzu ,iwapo Australia itashindwa kuilaza Peru. Denmark itaongoza kundi hilo kwa kupata ushindi.

Ili Australia kufuzu , lazima iishinde Peru ,huku ikutumai kwamba Denmark itapoteza mbali na kupata magoli mengi kuishinda .

Jumanne 26 Juni

Denmark v France, Uwanja wa Luzhniki, 15:00 BST

Australia v Peru, Uwanja wa Fisht Olympic, 15:00 BST

Mshindi wa Kundi atacheza na mshindi Kundi D, Namba mbili atacheza na mshindi Kundi D.

Group D

Image captionKUNDI D

Croatia imefuzu na watakuwa washindi wa kundi hilo iwapo watapata pointi moja dhidi ya Iceland.

Nigeria itafuzu iwapo itapata ushindi dhidi ya Argentina. Pointi moja itatosha iwapo Iceland haitaishinda Croatia.

Iwapo Argentina na Nigeria zitatoka sare, Iceland itafuzu iwapo itaishinda Croatia kwa mabao mawili na pia kufunga bao moja zaidi ya Nigeria.

Argentina itafuzu iwapo itailaza Nigeria huku nayo Iceland ikishinda kuilaza Croatia. Basi kikosi cha Jorge Sampaoli kitafuzu iwapo kitaishinda Nigeria kwa zaidi ya magoli mawili zaidi ya iwapo Iceland itashinda.

Iwapo Argentina na Iceland zitashinda na kumaliza na ushindani wa kufanana , hatma yao itaamuliwa na rekodi yao ya adhabu badala ya kupigiwa kura.

Jumanne 26 Juni

Nigeria v Argentina, Uwanja wa Krestovsky 19:00 BST

Iceland v Croatia, Rostov Arena, 19:00 BST

Mshindi wa Kundi anacheza na namba mbili Kundi C. Namba mbili atacheza na mshindi Kundi C.

Group E

Sare kati ya Brazil dhidi ya Serbia itatosha kuifanya ifuzu katika awamu ya muondoano

Iwapo Brazil na Uswizi zitashinda , mshindi wa kundi hilo huenda akaamuliwa kupitia rekosi za adhabu.

Brazil ina kadi tatu za njano , Switzerland nne. iwapo zote mbili zitapoteza basi timu itakayoshikilia nafasi ya tatu zitajulikana kupitia mbinu hiyohiyo.

Uswizi itafuzu kupitia sare dhidi ya Costa Rica, ama iwapo Serbia itapoteza kwa Brazil.

Iwapo Uswizi itapoteza kwa goli moja na Serbia kupata sare, nafasi ya pili itaamuliwa kupitia magoli yaliofungwa.

Iwapo pande zote zitamaliza na rekodi sawa , basi Uswizi itasonga mbele baada ya kuifunga Serbia.

Serbia itafuzu iwapo itailaza Brazil . Sare itatosha iwapo Uswizi itapoteza kwa Costa Rica kwa zaidi ya goli moja

Jumatano 27 Juni

Serbia v Brazil, Uwanja wa Otkritie, 19:00 BST

Switzerland v Costa Rica, Uwanja wa Nizhny Novgorod, 19:00 BST

Mshindi wa Kundi anacheza na namba mbili Kundi F. Namba mbili atacheza na mshindi Kundi F.

Kundi F

Image captionKUNDI F

Mexico inahitaji pointi moja dhidi ya Sweden ili kuweza kufuzu na kumaliza kileleni mwa kundi F .

Watasonga mbele licha ya ,matokeo yao yoyote yale iwapo Ujerumani itashindwa kuilaza Korea Kusini.

Sweden imehakikishiwa kufuzu iwapo itashinda matokeo ya Ujerumani.

Watakuwa kileleni mwa kundi hilo iwapo wataishinda Mexico na kupata matokeo mazuri zaidi ya Ujerumani.

Ujerumani itafuzu iwapo itashinda kwa zaidi ya magoli mawili ama hata zaidi.

Iwapo Ujerumani na Sweden zitatoka sare, basi timu itakayokuwa na magoli mengi itamaliza wa pili. Iwapo mechi zote zitamaliza na mabao sawa , basi Ujerumani itamaliza wa pili kwa sababu waliilaza Sweden.

Sweden itafuzu iwapo itashinda kwa zaidi ya magoli mawili zaidi.

Korea Kusini itafuzu iwapo itaishinda Ujerumani na Swedn kupoteza na kumaliza na tofauti nzuri ya magoli zaidi ya timu hizo mbili.

Jumatano, 27 Juni

South Korea v Germany, Kazan Arena, 15:00 BST

Mexico v Sweden, Uwanja wa Central, 15:00 BST

Mshindi wa Kundi anacheza na namba mbili Kundi E. Namba mbili atacheza na mshindi Kundi E.

KundiG

Uingereza na Ubelgiji zimefuzu na zina rekodi sawa zikisalia na mechi moja ya mwisho.

Iwapo zitatoka sare , nafasi mbili za kwanza zitaamuliwa na idadi ya kadi za adhabu zilizotolewa kwa timu hizo mbili .

Uingereza ina kadi mbili za njano huku Ubelgiji ikiwa na kadi tatu. Iwapo timu zote mbili zitakuwa na idadi sawa ya kadi basi zitapigiwa kura kuamua.

Group H

Japan na Senegal zinahitaji pointi moja moja zote mbili katika mechi zao za mwisho dhidi ya Poland na Colombia kufuzu.

Colombia itafuzu kupitia ushindi dhidi ya Senegal.

Iwapo Colombia itaishinda Japan italazimika kupoteza kwa mabao machache zaidi ya Senegal ili kusonga mbele.

Colombia pia inaweza kufuzu kupitia sare iwapo Japan itapoteza kwa sababu ina wingi wa tofauti ya mabao.

Alhamisi 28 Juni

England v Belgium, Uwanja wa Kaliningrad, 19:00 BST

Panama v Tunisia, Mordovia Arena, 19:00 BST

Mshindi wa Kundi anacheza na namba mbili Kundi H. Namba mbili atacheza na mshindi Kundi H.

Alhamisi, 28 Juni

Japan v Poland, Volgograd Arena, 15:00 BST

Senegal v Colombia, Samara Arena, 15:00 BST

Mshindi wa Kundi anacheza na namba mbili Kundi G. Namba mbili anacheza na mshindi Kundi G.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post