Baada ya klabu za Yanga na St George
kujitoa kwenye michuano ya kombe la Kagame inayoanza wiki ijayo, Juni
28, CECAFA imetoa ratiba mpya ya michuano hiyo.
CECAFA imeziongeza klabu za Singida United na APR kundi C kuungana na Simba na Dakadaha.
Vipers FC imepelekwa kundi A kuungana na Azam FC, JKU na Kator FC.
Kundi B limebaki na timu za Rayon Sport, Gor Mahia, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djibouti.
Mechi za ufunguzi zitachezwa Ijumaa ya Juni 29, kati ya JKU na Vipers Saa 8:00 mchana, Azam FC na Kator Saa 10:00 jioni na Singida United dhidi ya APR Saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam
Jumamosi ya Julai 30 kutakuwa na mechi mbili, Ports dhidi ya Lydia Saa 8:00 mchana na Simba dhidi ya Dakadaha Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa.