TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO 23 MEI 2018

Pep Guardiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anatathmini kumwinda mchezaji wa Ajax raia wa Uholanzi Matthijs de Ligt,18. (Guardian)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anafikiria kuchukua likizo kutoka kandanda ikiwa atafutwa na klabu hiyo. Telegraph)


Anthony MartialHaki miliki ya pichaPA
Image captionAnthony Martial

Manchester United wana nia ya kusikiliza ofa kwa mshambuliaji raia wa Ufaransa Anthony Martial, 22, lakini wako makini wasije wakamuuza kwenda klabu pinzani ya England. (Mail)
AC Milan wana mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Chelsea rai wa Uhispania Alvaro Morata, 25. (Sky Italia - in Italian)


Unai EmeryHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUnai Emery

Unai Emery hatakuwa na ushawishi katika kuwanunua na kuwauza wachezaji wakati atateuliwa meneja wa Arsenal. (Mirror)
Emery ana nia ya kumweka kiungo wa kati Aaron Ramsey, 27, katika mipango yake licha mchezaji huyo kuhusishwa na mpango wa kukihama klabu hiyo. (Sky Sports)


Mikel ArtetaHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionMikel Arteta

Kocha msaidizi Mikel Arteta anafanya makubaliano na Manchester City baada ya kushindwa kupata kazi huko Arsenal. (Telegraph)
Arsenal wanapanga kumsaini kiungo wa kati wa Nice raia wa Ivory Coast Jean Michael Seri, 26. (Mail)
Arsenal, Chelsea na Everton wote wanammezea mate mlinzi wa Hamburg mjerumani Josha Vagnoman 17. (ESPN)


Carlo AncelottiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionCarlo Ancelotti

Meneja wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Carlo Ancelotti amefanya mazungumzo na raia wa Napoli kuhusu kuchukua mahala pake Maurizio Sarri. (Sky Sports)
Swansea wamefanya mazungumzo na meneja wa Ostersunds FK, Graham Potter kuhusu nafasi iliyo wazi wa umeneja. (Mail)


Moussa SissakoHaki miliki ya pichaPA
Image captionMoussa Sissako

Meneja wa New York City na kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira amekana ripoti kuwa anapanga kujiunga an Nice kama meneja. (Goal)
Brighton wanakaribia kumsaini mlinzi wa Paris St-Germain raia wa Mali Moussa Sissako, 17. (RMC- via Mirror)
Bora kutoka Jumanne
Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, amesema wazi wazi anatataka kuondoka Real Madrid msimu huu wa joto , mwaka mmoja baada ya Mbrazil huyo kujiunga na mabingwa hao wa Ufaransa. (Goal)
Chelsea wamemuorodhesha mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 29, miongoni mwa wanaowataka kuwasajili msimu huu. (Telegraph)
Manchester United wanamatamanio ya kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Willian, 29, msimu huu wa uhamisho. (Sky Sports)


NeymarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNeymar

Lakini Manchester United wako tayari kujiondoa kwa uhamisho wa £53m wa Shakhtar Donetsk na kiungo wa kati wa Brazil Fred ,25. (Metro)
Mshambuliaji wa kimataifa wa Manchester United Anthony Martial, 22, ananyemelewa na mahasimu wao wa ligi ya Premia Tottenham. (London Evening Standard)
Barcelona wanapanga kusamjili mshambuliaji wa Spurs Reo Griffiths katika uhamisho wa msimu huu wa joto. (Star)



Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post